Friday, November 21, 2008

Soo la Juma Nature

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Juma Kassimu 'Nature' (28) anakabiliwa na shitaka la kubaka msichana aliye na umri wa miaka (16) kwa zamu. Akiwasomea mashitaka hayo mwendesha mashitaka wa mahakama ya wilaya ya Temeke Bw. Basall Pandisha alidai kuwa, mnamo Novemba mosi mwaka huu majira ya saa 1 jioni katika eneo maarufu lijulikanalo kama 'Sugar Rays' lililopo wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salam, Nature na mwenzake aliyetambulika kwa jina la Godwin Malima (26) ambaye ni mwalimu, walimbaka kwa zamu msichana huyo mwenye umri wa chini ya miaka 18.

Aidha, mwendesha mashitaka huyo alidai kuwa shitaka la pili ni kwa mtuhumiwa wa pili Bw. Godwin ambalo ni kumtorosha msichana huyo na kwenda kuishi naye bila ridhaa ya wazazi wake.

Kesi hiyo inatarajiwa kusomwa tena mwanzoni mwa mwezi wa Desemba mwaka huu.

No comments: