Kupitia hapa utaweza kupata Habari mbalimbali zikiwemo za Siasa, Michezo, Biashara, Dini, Mapenzi, Afya, Mazingira na mambo mengi yanayomzunguka mwanadamu.
Wednesday, November 5, 2008
Baada ya kutangazwa Ushindi wa Obama..
Raisi mtarajiwa wa Marekani Bw. Barack Obama na Mke wake Michelle Obama wakiondoka ktk mkutano wa kutoa shukurani zao kwa wapiga kura wa Chicago kwa kufanikisha ushindi wa chama chake katika jiji hilo..
Mama huyu wa jiji la New York akilia katika kule kutoamini kama kweli Obama ameibuka kidedea..
Mamia ya wafuasi wa Bw. Obama wakipigwa na Butwaa huku wengine wakiwa na furaha kwa kutoamini ushindi wa mgombea wao..
Nao wakazi wa Kibera nchini Kenya wakifurahia ushindi huo huku wakipeperusha bendera ya Marekani, Kenya ndio asili ya baba yake Obama, Marehemu Barack Hussein Obama..
Mamia ya wafuasi wa Barack Obama wengi wao wakiwa na asili ya weupe wakifurahia ushindi wa mgombea wao.
Raisi mtarajiwa wa Marekani kutoka chama cha Demokratik Bw. Barack Obama akiwa amekumbatiana na mkewe Michelle huku makamu wake Bw. Joe Biden na mkewe wakiwa wamekumbatiana pembeni yao katika kujipongeza kutokana na kuibuka washindi katika kinyang'anyiro cha uraisi nchini humo.
Raisi wa Afghan Bw. Hamid Karzai akiongea na waandishi wa habari ndani ya makazi ya Raisi mjini Kabul, Afghanistan, Jumatano, Nov. 5, 2008. Karzai alisema uteuzi wa Barack Obama kama raisi wa kwanza mweusi wa Marekani ni kiashirio cha wakati mzuri kwa Marekani na Dunia kiujumla..
No comments:
Post a Comment