Tuesday, November 11, 2008

ATR ya Precision Air

Shirika binafsi la Ndege Precision Air, Leo limezindua ndege aina ya ATR itakayofanya safari zake kati ya Dar - Mwanza - Musoma , uzinduzi huo umefanyika leo katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere uliopo hapa jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na baadhi ya wadau wa shirika hilo, Ndege hiyo inauwezo wa kubeba abiria 76.
Ndege yenyewe aina ya ATR ikiwa ndani ya Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere asubuhi ya leo..

Mdau wa wa kampuni hiyo Bw. Michael Shirima, akikata utepe kuzindua ndege hiyo, Kutoka kulia ni muongoza ndege wa siku nyingi Bw. Makinda, akifuatiwa na Bw Shirima (anayekata utepe) Nyuma anayepiga makofi ni muwakilishi toka Shirika la Ndege la Kenya Bw. Emanuel akifuatiwa na Meneja wa kampuni hiyo Bw. Kioko

Wakionekana kupongezana ndani ya ndege hiyo, wa mbele kulia ni Bw. Shirima kushoto ni Kioko, Nyuma kulia ni mwakilishi kutoka shirika la ndege la Kenya Ndg. Emanuel wakipeana mikono na Bw. Makinda.

No comments: