Wale Wasabato 'Masalia' leo wameibuka tena katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere 'Terminal II' wakitaka kusafiri bila hati za kusafiria, tiketi, mualiko na hata wanakotaka kwenda hakujajulikana, Wasabato hao wapatao thelathini waliibuka ndani ya uwanja huo kunako majira ya saa 1 asubuhi ya leo wakiwemo akina mama na watoto kadhaa, wana usalama wa uwanja huo ilibidi watumie busara bila nguvu kuwachukua na kuwapeleka katika kituo cha Polisi kilichopo uwanja wa ndege wa zamani 'Terminal I' kwa mahojiano zaidi.
Wakiwa wamebarizi kusubiri muda wa ku-check in
Hapa ni baada ya kuamriwa kuondoka katika uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere na kutakiwa kuelekea Uwanja wa ndege wa zamani kutoa maelezo
Wakipandishwa ndani ya gari la usalama wa raia huku wakiwa wamesimamiwa na wana usalama wa uwanjani hapo
Kundi la akina mama wakisabato 'Masalia' nao hawakuachwa nyuma na wanausalama
Gari ya pili ikichukua baadhi ya Wasabato waliosalia uwanjani hapo
Wakielekea kituo cha Polisi kilichopo katika uwanja wa Ndege wa zamani 'Terminal I' huku wakijifariji kwa nyimbo na mapambio.
No comments:
Post a Comment