Washindi katika tuzo maarufu zijulikanazo kama 'Pam Awards' zilizofanyika nchini Uganda jumamosi iliyopita pale Shimoni Grounds.AY ameibuka mshindi katika kipengele cha Best Male Artist-Tanzania ambapo alikuwa sambamba na wasanii wengine maarufu wa nchini Tanzania kama vile Prof Jay, Mr.Nice na Bushoke huku Lady Jay Dee akiibuka Best Female Artist kutoka Tanzania.

NB: AY (pamoja na MwanaFA) wameteuliwa kuwania KISIMA AWARDS ambazo ni tuzo maarufu za nchini Kenya. Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika tarehe 29 November 2008 jijini Nairobi. AY na MwanaFA wamechaguliwa kuwania tuzo hizo katika kipengele cha Best Video -Tanzania kupitia video yao ya Nangoja Ageuke.
No comments:
Post a Comment