Monday, November 3, 2008

Mbinu mpya ya kuzuia Uhalifu wa Kimtandao

Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Bw. Suleimani Kova amesema jeshi hilo limejizatiti katika kukabiliana na mbinu mpya zinazofanywa na wahalifu wanaotumia mitandao ya kompyuta. Hatua hiyo ya jeshi la polisi imekuja kufuatia kuibuka kwa wimbi la watu wanaotumia mitandao ya kompyuta kuchafua watu ambapo amesema polisi imeamua kufungua barua pepe ambayo itatumika katika kukabiliana na uhalifu wa aina hiyo.

No comments: