Serikali imekifunga Chuo kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya mlimani na kuwataka wanafunzi wote wanaochukua shahada ya kwanza kuondoka chuoni hapo haraka, taarifa ya kufungwa Chuo hicho imetolewa na makamu mkuu wa Chuo hicho Prof. Rwekaza Mkandala na kubandikwa kwenye mbao za matangazo chuoni hapo majira ya saa 5 leo asubuhi.
Tangazo hilo liliwataka wanafunzi wote wanaochukua shahada ya kwanza kukusanya vifaa vyao na kuachia vyumba haraka bila kufafanua zaidi nini kitakachoendelea na kufafanua kwamba watakaobaki chuoni hapo ni wale wanaochukua shahada ya pili na kuendelea, wanafunzi wa kozi fupi na wale wa kigeni.
Maamuzi haya yamekuja baada ya kufanyika kwa maandamano mara tatu mfululizo kutoka kwa wanafunzi hao wakidai wapatiwe asilimia mia moja ya mikopo ya elimu ya juu badala ya ile arobaini ya awali..
Maamuzi haya yamekuja baada ya kufanyika kwa maandamano mara tatu mfululizo kutoka kwa wanafunzi hao wakidai wapatiwe asilimia mia moja ya mikopo ya elimu ya juu badala ya ile arobaini ya awali..
No comments:
Post a Comment