Monday, November 10, 2008

Mama Afrika 'Miriam Makeba' Afariki..

Mwanamuziki nguli kutoka Afrika ya Kusini 'Miriam Makeba (76)' amefariki mapema jumapili huko mjini Italia alikokuwa kwa ajili ya onyesho, msemaji wa mwana mama huyo amedai mwanamuziki huyo amefariki katika kliniki ya Pineta Grande iliyopo Castel Volturno, Italia.

Habari kutoka vyombo mbalimbali vya Italia vimedai mwanamuziki alifariki muda mchache baada ya kufikishwa katika kliniki hiyo.

Miriam Makeba, alipatwa na mshtuko wa moyo mara tu baada ya kufanya onyesho ambapo aliimba kwa takribani dakika thelathini kuonyesha mshikamano miongoni mwa waandishi wa habari wa kiitalia, baada ya mwandishi mwenzao Roberto Saviano kupokea vitisho baada ya kuandika kitabu kuhusiana na Camorra, Naples eneo lijulikanalo kama kitovu cha uhalifu.

Makeba alianza kutambulika kimataifa mara baada ya kutoka na dokomentari yake iliyojulikana kama 'Come Back Afrika' mnamo mwaka 1959, na Mwaka 1960 baada ya kuzuiwa alipokuwa akirudi kwa ajili ya kushiriki mazishi ya mama yake baada ya hati yake ya kusafiria kuwa na hitilafu. Mwaka 1966 Makeba alipokea tuzo za Grammy kupitia kibao 'An Evening with Belafonte/Makeba' alichoshirikiana na Harry Belafonte.

Taarifa ya kifo cha 'Makeba' imeshtua raia wengi wa Afrika ya Kusini, Afrika na Dunia kiujumla.


MUNGU AILAZE ROHO YA MAMA AFRIKA 'MIRIAM MAKEBA' MAHALI PEMA PEPONI AMEN

No comments: