Monday, November 17, 2008

1955 Land Rover 107 Pick-up

Hii ni Land Rover 107 ya mwaka 1955, Usafiri huu ulitumika kuanzia mwaka huo wa 1955 mpaka mwanzoni mwa miaka ya 1970 ambapo iliondolewa katika chati na toleo 3 ambapo ndio lilikuwa toleo jipya la Land Rover miaka hiyo. Toleo hilo la 3 lilikaa sokoni kwa takribani miaka ishirini kuanzia miaka hiyo ya 70 mpaka mwanzoni mwa miaka ya 90. Kwa wale wazaliwa wa zamani lazima watakuwa na kumbukumbu nzuri sana na aina hii ya gari kwani kwa miaka hiyo ulikuwa ndio usafiri wa gharama sana uliokuwa ukitumika zaidi na kwa shughuli za serikali nyingi karibu duniani kote.

Hapa ikionekana kwa mbeleJustify Full
Ndani ilikuwa simpo sana yaani hata mziki na kiyoyozi vilionekana kama anasa, na havikuwa vitu vya msingi sana zaidi ya mlio wa mashine na joto la kufa mtu..

Hapa ikionekana kwa nyuma, kwa wale vijana wa zamani na michezo yao ya kudandia hapa ilikuwa ni burudani tu..

No comments: