Wednesday, November 5, 2008

OBAMA 'Changes has Come to America'

Barack Obama akipungia mkono mamia ya wafuasi wake huku akiwa na Mkewe pamoja na watoto wao katika moja ya kampeni zake za kuwania uraisi wa Marekani, Seneta huyo ameibuka kinara katika kinyang'anyiro hicho kilichokuwa na upinzani mdogo dhidi ya mpinzani wake John McCain kutoka chama cha raisi anayeondoka madarakani Bw. George Walker Bush.

Hatimaye mkenya, Seneta Barack Obama wa chama cha Demokrati cha atinga katika ikulu za marekani, Bw. Obama anaweka historia ya kuwa Mwafrika wa kwanza kuingia katika Ikulu za Marekani maarufu kama 'White House' akiwa raisi wa arobaini na nne (44) kwa Taifa hilo lililo na nguvu zaidi duniani, Obama anaweka historia ya iliyokuwa 'ndoto' ya wanaharakati wengi waki-Afrika akiwemo Martin Luther King Jr na Malcolm 'X' ambao hawakuwahi kutimiza ndoto hiyo waliyoipigania katika kipindi chote cha Uhai wao..

No comments: