Sunday, November 30, 2008

Chadema na walia na kufungwa faili la Karamagi

WAKATI Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) imefunga faili la uchunguzi dhidi ya waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi.

Habari kutoka kwenye ofisi ya DPP na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) zinasema vielelezo vilivyowasilishwa havikuwa na nguvu za kumfikisha Karamagi mbele ya mkono wa sheria.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, maoni ya ofisi ya DPP ni kwamba mbunge huyo wa Bukoba Vijijini alifuata ushauri wa watalaam kusaini mkataba huo, licha ya kwamba tarehe ambayo alipokea ushauri huo ndiyo aliyosafiri kwenda London, Uingereza kusaini mkataba huo.

Big Brother Africa III '08'


Shindano la Big Brother Africa III limemalizika usiku wa kuamkia leo huko Afrika Kusini ambapo kijana Ricardo David Ferreira Venancio a.k.a Ricco kutoka Angola, (21) ndio mshindi wa shindano la mwaka huu.
Tofauti na mashindano mengine, shindano la mwaka huu lilibidi liamuliwe kwa kutafuta asilimia ya jumla ya kura zote zilizopigwa mwaka huu baada ya Ricco kufungana na binti kutoka Malawi, Hazel(25)

Tuesday, November 25, 2008

Sakata la migomo Vyuo vikuu na Kauli ya Rais

Kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuwa serikali yake haikubaliani na matakwa ya wanafunzi kudai wakopeshwe asilimia 100 ya gharama za masomo, imepokelewa kwa hisia tofauti na wanasiasa wakieleza kuwa kwa msimamo huo taifa linaelekea gizani na kwamba athari zake hazitakawia.

Serikali imefunga vyuo vyake saba kutokana na wanafunzi kugoma kuingia madarasani wakishinikiza sera ya uchangiaji elimu ibadilishwe na kama itaendelea, basi wanafunzi wakopeshwe kwa asilimia mia badala ya mpango wa sasa (means testing) ambao huchambua uwezo wa familia ya mwanafunzi na kuwapanga kwa makundi.

Vyuo vilivyofungwa ni Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu (Duce), Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara (MUCCOBS), Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, Chuo Kikuu Kishiriki cha Ardhi, Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa na Taasisi ya Teknolojia ya Dar es salaam (DIT).

Tembelea hapa

Mabadiliko ya awamu ya Nne

Serikali ya awamu ya nne, imeamua kuachana na magari iliyotumia kwa muda mrefu ya Marcedes Benz na sasa inatumia magari mengine ya kifahari ya BMW kwa ajili ya msafara wa rais.

Mercedes Benz, gari ya kifahari inayotengenezwa nchini Ujerumani, imekuwa ikitumiwa na serikali zote tatu zilizopita zilizoongozwa na Mwalimu Julius K. Nyerere, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa. Gari iliyotumika mwanzoni mara baada ya kupata uhuru ilikuwa Rolls Royce.

Lakini kwa sasa, msafara wa Rais unapambwa na magari matano ya BMW, mawili yakiwa ni X 5, ambayo ni mithili ya Toyota VX kwa ukubwa na matatu yakiwa Series Seven

Chini ni mifano ya gari hizo..

Hii ndio BMW Seven Series

BMW X 5

Friday, November 21, 2008

Katibu wa Vyuo Vikuu kizimbani

Katibu Mkuu wa chama cha wanafunzi wa vyuo vikuu nchini, Bw. Julius Mtatiro akiwa kizimbani kwa tuhuma zinazomkabili za kuhamasisha mgomo katika Chuo Kikuu Dar es Salaam, chama wanafunzi wa shuleni hapo 'DARUSO' kimenyetisha kuwa jamaa amewekewa dhamana mpaka kesi yake itakapotajwa tena Dec. 2 mwaka huu.

Soo la Juma Nature

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Juma Kassimu 'Nature' (28) anakabiliwa na shitaka la kubaka msichana aliye na umri wa miaka (16) kwa zamu. Akiwasomea mashitaka hayo mwendesha mashitaka wa mahakama ya wilaya ya Temeke Bw. Basall Pandisha alidai kuwa, mnamo Novemba mosi mwaka huu majira ya saa 1 jioni katika eneo maarufu lijulikanalo kama 'Sugar Rays' lililopo wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salam, Nature na mwenzake aliyetambulika kwa jina la Godwin Malima (26) ambaye ni mwalimu, walimbaka kwa zamu msichana huyo mwenye umri wa chini ya miaka 18.

Aidha, mwendesha mashitaka huyo alidai kuwa shitaka la pili ni kwa mtuhumiwa wa pili Bw. Godwin ambalo ni kumtorosha msichana huyo na kwenda kuishi naye bila ridhaa ya wazazi wake.

Kesi hiyo inatarajiwa kusomwa tena mwanzoni mwa mwezi wa Desemba mwaka huu.

Baada ya Obama sasa ni Eric Holder

Vyombo mbambali vya habari nchini Marekani vimeripoti kuwa raisi mteule wa Marekani Bw. Barack Obama amempendekeza Bw. Eric Holder kuwa waziri wa ulinzi wa taifa hilo, Bw. huyo (Eric Holder) alikuwa makamu waziri wa ulinzi wakati wa kipindi cha Rais Bill Clinton, Na endapo atachaguliwa na kuapishwa na bunge la nchi hiyo, Eric Holder aliye na rekodi nzuri katika nyadhifa nyingi alizowahi kushikilia, atakuwa ndio m-marekani mweusi wa kwanza kuwa waziri wa Ulinzi wa Taifa hilo lililo na nguvu kubwa kiuchumi Duniani.

Monday, November 17, 2008

Mbinu za kuacha Uvutaji

Katika pitapita zangu mtandaoni nilibahatika kukutana hili nikaona si vibaya kama tutaliona pamoja..

HOW TO QUIT SMOKING?

1. Believe in itself. Believe, that you can throw. Recollect the most difficult things by which you did and realize, that you have will power and determination to stop to smoke. All depends on you.

2. After you reading this list, sit down and write, advanced according to your character traits and features. Create the own plan how to stop to smoke.

3. Commit to paper the reasons on which you wish to stop to smoke (advantages of a life without smoking): to live longer, to feel better, for the family, to save up money, to smell better, easier to find pair, etc. you know, that bad in smoking and that you we shall get having stopped. Write down all on a paper and read daily.

4. Ask the family and friends to support you in your decision to stop to smoke. Ask them about complete support and tolerance. Let them know in advance, that you, probably, will be irritable even irritating during parting with this bad habit.

5. Appoint a date closed of smoking. Solve, in what day you stops smoking with cigarettes for ever. Write down this date. Plan it{her}. Prepare the brain for « the first day of your new life ». You even can lead small ceremony in occasion of your last cigarette or morning of day of refusal of smoking.

6. Talk to your doctor in occasion of refusal to smoke. Support and an orientation received from the doctor - the checked up way to improve your chances of success.

7. Sports are simply incompatible with smoking. Exercises remove stress and help{assist} your body to be restored from harm put{rendered} by cigarettes. If it is necessary, begin gradually, with short walk of times or two in day. Finish it till 30-40 minute exercises 3 or 4 times a week. Consult to the doctor before will begin any exercises.

8. Do deep respiratory exercises every day for 3-5 minutes. Very slowly inhale through a nose, hold the breath for some seconds, very slowly exhale through a mouth. Try to do respiratory exercises blindly and pass to п.9

9. Clearly imagine, as you will cease to be the smoker. During respiratory exercises п.8 you can close eyes and imagine yourselves non-smoking. You should see yourselves enjoying exercises п.7. Present itself refusing from the offered cigarette. See, how you throw out all the cigarettes away and receiving for it a gold medal. Develop own creative representations. “Visualization” will work.

10. Reduce quantity of cigarettes gradually (if you reduce quantity of cigarettes, necessarily appoint{nominate} day of FINAL refusal of smoking). Ways of gradual refusal of smoking include: planning of quantity of smoked cigarettes on every day before the ending of smoking, reduction of quantity of smoked cigarettes every day, purchase of cigarettes in quantity of no more than one pack, replacement of mark that not so process of smoking liked. Give the cigarettes to somebody to another that you had to ask each time them when you want to smoke.

11. Try “to fasten” - to stop to smoke once and for all. Many smokers have checked up on themselves, that a unique way to leave cigarettes - to throw sharply and completely, without attempts to reduce quantity of smoked cigarettes. Nevertheless, find a method which will be the most suitable for you: to throw gradually or at once. If one of methods will not work - try another.

12. Find to itself the partner - other smoker who also wishes to stop to smoke. Encourage and assist each other, address to the friend when will feel that do not maintain. Come to us on the Forum or into a chat, there for certain there will be a help.

13. Carefully clean a teeth. Pay attention to how their condition quickly improves and as they grow white. Imagine and take pleasure from an idea on how they will look in a month, three or year.

14. After you have stopped to smoke, plan to note round dates on your way from smoking to non-smoking. In 2 weeks - descend at cinema. In a month - descend in good restaurant or in cafe (necessarily sit down in section for non-smoking!). In 3 months - lead days off in your favourite place. In 6 months - buy to itself something serious. In 1 year arrange to itself a party. Will invite the family and friends to “birthday” of the person which has got chance to live a long and healthy life.

15. Drink a lot of water. Water is good in any case and the majority of people do not drink it in enough. Water will help “to wash up” nicotine and other chemistry from an organism, besides it will help to remove bent for to cigarettes, answering on ” inquiries of a mouth “.

16. Realize, during what time you have a desire to smoke, for example: during stress, after meal, during arrival for work, etc. Try to avoid these situations and if it is impossible - find other models of behaviour during these moments.

17. Find something, that it is possible to hold in a hand and in a mouth what to replace with it cigarettes. Try to use tubes for drink, can as to try substitutes of cigarettes named ” E-Z Quit ”. The additional information can be found here.

18. Write a good song or a verse on a theme « I Stop to smoke », about cigarettes, and that for you means to leave tobacco. Read it every day.

19. Carry with itself a photo of the family or the one who to you of roads. Write on a sheet of a paper: ” I throw for myself and for you (you) ” and attach it to a photo. When you will have a desire to smoke, look at a photo and read an inscription.

20. Each time when you have a desire to smoke, instead of what to smoke write down the feelings or everything, that at you on mind. Carry this sheet always with itself.

21. Use the specialized medical products preventing bent for to nicotine, for example Nirdosh, Wellbutrin SR, Zyban, Zero Nicotine, Nicotinell.

Visit: http://professionalmedicines.com

We wish good luck in your aspiration to stop to smoke. It is that costs!

Kwaherini.

1955 Land Rover 107 Pick-up

Hii ni Land Rover 107 ya mwaka 1955, Usafiri huu ulitumika kuanzia mwaka huo wa 1955 mpaka mwanzoni mwa miaka ya 1970 ambapo iliondolewa katika chati na toleo 3 ambapo ndio lilikuwa toleo jipya la Land Rover miaka hiyo. Toleo hilo la 3 lilikaa sokoni kwa takribani miaka ishirini kuanzia miaka hiyo ya 70 mpaka mwanzoni mwa miaka ya 90. Kwa wale wazaliwa wa zamani lazima watakuwa na kumbukumbu nzuri sana na aina hii ya gari kwani kwa miaka hiyo ulikuwa ndio usafiri wa gharama sana uliokuwa ukitumika zaidi na kwa shughuli za serikali nyingi karibu duniani kote.

Hapa ikionekana kwa mbeleJustify Full
Ndani ilikuwa simpo sana yaani hata mziki na kiyoyozi vilionekana kama anasa, na havikuwa vitu vya msingi sana zaidi ya mlio wa mashine na joto la kufa mtu..

Hapa ikionekana kwa nyuma, kwa wale vijana wa zamani na michezo yao ya kudandia hapa ilikuwa ni burudani tu..

Sunday, November 16, 2008

Kaseba amchapa King Unishiro

Bingwa wa ligi ya ngumi inayojulikana kama 'K1' Japhet Kaseba, Amewasili jana akitokea nchini Japa, Japhet alimchapa mpinzani/mwenyeji wake mjapani King Unishiro katika pambano lililofanyika nchini humo.

Vitisho dhidi ya Obama


Vitisho dhidi ya raisi mteule wa Marekani bwana Barack Obama vimeripotiwa kuzidi kuongezeka tangu aibuke mshindi katika kinyang'anyiro hicho kilichofanyika Novemba 4 mwaka huu, Ingawa vyombo vya usalama wa viongozi havikubainisha idadi ya kesi zinahozusu vitisho hivyo, Taarifa zilizopo kutoka ndani ya vyombo hivyo zinaeleza kuwa wamekuwa akigundua mipango mingi kupitia maandishi na barua pepe! Wana usalama hao pia wamedai kugundua mambo mengine ambayo yamekuwa yakitoa maelekezo kuhusu mipango michafu dhidi ya Obama tofauti na viongozi waliotangulia..

Aidha vyombo vya habari vya Merekani vimesema kuwa Raisi huyo mteule amekuwa na mkutano na aliyekuwa hasimu wake ktk kinyang'anyiro cha kuwania kuteuliwa kuwa mgombea nafasi ya Urais kwa tiketi ya chama cha Demokratik, Hillary Clinton, akitaka kumteuwa katika wadhifa wa ngazi ya juu katika utawala wake.

Thursday, November 13, 2008

Sakata la Wasabato Masalia laibuka tena Airport

Wale Wasabato 'Masalia' leo wameibuka tena katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere 'Terminal II' wakitaka kusafiri bila hati za kusafiria, tiketi, mualiko na hata wanakotaka kwenda hakujajulikana, Wasabato hao wapatao thelathini waliibuka ndani ya uwanja huo kunako majira ya saa 1 asubuhi ya leo wakiwemo akina mama na watoto kadhaa, wana usalama wa uwanja huo ilibidi watumie busara bila nguvu kuwachukua na kuwapeleka katika kituo cha Polisi kilichopo uwanja wa ndege wa zamani 'Terminal I' kwa mahojiano zaidi.

Wakiwa wamebarizi kusubiri muda wa ku-check in

Hapa ni baada ya kuamriwa kuondoka katika uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere na kutakiwa kuelekea Uwanja wa ndege wa zamani kutoa maelezo


Wakipandishwa ndani ya gari la usalama wa raia huku wakiwa wamesimamiwa na wana usalama wa uwanjani hapo

Kundi la akina mama wakisabato 'Masalia' nao hawakuachwa nyuma na wanausalama

Gari ya pili ikichukua baadhi ya Wasabato waliosalia uwanjani hapo



Wakielekea kituo cha Polisi kilichopo katika uwanja wa Ndege wa zamani 'Terminal I' huku wakijifariji kwa nyimbo na mapambio.

Wednesday, November 12, 2008

Mtafaruku wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Serikali imekifunga Chuo kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya mlimani na kuwataka wanafunzi wote wanaochukua shahada ya kwanza kuondoka chuoni hapo haraka, taarifa ya kufungwa Chuo hicho imetolewa na makamu mkuu wa Chuo hicho Prof. Rwekaza Mkandala na kubandikwa kwenye mbao za matangazo chuoni hapo majira ya saa 5 leo asubuhi.

Tangazo hilo liliwataka wanafunzi wote wanaochukua shahada ya kwanza kukusanya vifaa vyao na kuachia vyumba haraka bila kufafanua zaidi nini kitakachoendelea na kufafanua kwamba watakaobaki chuoni hapo ni wale wanaochukua shahada ya pili na kuendelea, wanafunzi wa kozi fupi na wale wa kigeni.

Maamuzi haya yamekuja baada ya kufanyika kwa maandamano mara tatu mfululizo kutoka kwa wanafunzi hao wakidai wapatiwe asilimia mia moja ya mikopo ya elimu ya juu badala ya ile arobaini ya awali..

Askari wa kutuliza ghasia (FFU) maarufu kama 'fanya fujo uone' wakiwa katikati ya wanachuo hao katika kufuatilia hali ya usalama miongoni mwa wanachuo..

Mamia ya wanachuo katika maandamano yaliyosababisha kufungwa kwa chuo hicho bila kufahamika nini kitafuatia baada ya tukio hilo..

Wanachuo wakiwa katika harakati za kupigania haki zao..

Tuesday, November 11, 2008

TID akata Rufaa

Mwanamuziki wa kizazi kipya T.I.D ambaye hivi karibuni imetoa singo yake mpya iliyo na ujumbe mzito inayoenda kwa jina la 'SIWEZI' hatimaye ameamua kukata rufaa kuhusiana na kesi inayomkabili, Khalid Mohamed a.k.a T.I.D leo asubuhi ametinga mahakamani kueleza adhma yake ya kutaka kukata rufaa kutokana na kifungo cha mwaka mmoja alichohukumiwa yapata miezi minne iliyopita.

ATR ya Precision Air

Shirika binafsi la Ndege Precision Air, Leo limezindua ndege aina ya ATR itakayofanya safari zake kati ya Dar - Mwanza - Musoma , uzinduzi huo umefanyika leo katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere uliopo hapa jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na baadhi ya wadau wa shirika hilo, Ndege hiyo inauwezo wa kubeba abiria 76.
Ndege yenyewe aina ya ATR ikiwa ndani ya Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere asubuhi ya leo..

Mdau wa wa kampuni hiyo Bw. Michael Shirima, akikata utepe kuzindua ndege hiyo, Kutoka kulia ni muongoza ndege wa siku nyingi Bw. Makinda, akifuatiwa na Bw Shirima (anayekata utepe) Nyuma anayepiga makofi ni muwakilishi toka Shirika la Ndege la Kenya Bw. Emanuel akifuatiwa na Meneja wa kampuni hiyo Bw. Kioko

Wakionekana kupongezana ndani ya ndege hiyo, wa mbele kulia ni Bw. Shirima kushoto ni Kioko, Nyuma kulia ni mwakilishi kutoka shirika la ndege la Kenya Ndg. Emanuel wakipeana mikono na Bw. Makinda.

Monday, November 10, 2008

Mama Afrika 'Miriam Makeba' Afariki..

Mwanamuziki nguli kutoka Afrika ya Kusini 'Miriam Makeba (76)' amefariki mapema jumapili huko mjini Italia alikokuwa kwa ajili ya onyesho, msemaji wa mwana mama huyo amedai mwanamuziki huyo amefariki katika kliniki ya Pineta Grande iliyopo Castel Volturno, Italia.

Habari kutoka vyombo mbalimbali vya Italia vimedai mwanamuziki alifariki muda mchache baada ya kufikishwa katika kliniki hiyo.

Miriam Makeba, alipatwa na mshtuko wa moyo mara tu baada ya kufanya onyesho ambapo aliimba kwa takribani dakika thelathini kuonyesha mshikamano miongoni mwa waandishi wa habari wa kiitalia, baada ya mwandishi mwenzao Roberto Saviano kupokea vitisho baada ya kuandika kitabu kuhusiana na Camorra, Naples eneo lijulikanalo kama kitovu cha uhalifu.

Makeba alianza kutambulika kimataifa mara baada ya kutoka na dokomentari yake iliyojulikana kama 'Come Back Afrika' mnamo mwaka 1959, na Mwaka 1960 baada ya kuzuiwa alipokuwa akirudi kwa ajili ya kushiriki mazishi ya mama yake baada ya hati yake ya kusafiria kuwa na hitilafu. Mwaka 1966 Makeba alipokea tuzo za Grammy kupitia kibao 'An Evening with Belafonte/Makeba' alichoshirikiana na Harry Belafonte.

Taarifa ya kifo cha 'Makeba' imeshtua raia wengi wa Afrika ya Kusini, Afrika na Dunia kiujumla.


MUNGU AILAZE ROHO YA MAMA AFRIKA 'MIRIAM MAKEBA' MAHALI PEMA PEPONI AMEN

Sunday, November 9, 2008

Kat Deluna

Kat Deluna akiongea na waandishi wa Habari katika viwanja vya Leader lilikofanyika tamasha la utamaduni wa muziki 'Fiesta Jirambe 08'

Msanii toka ughaibuni Kat Deluna alipowasili katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Mwalimu Nyerere jijini Dar, msanii huyu amekonga nyoyo za watanzania walio wengi ktk tamasha la Fiesta Jirambe..

Vigogo wa EPA aibuni..


Hawa ndio baadhi ya wadaiwa wa utafunaji wa Fedha zilizokuwa za akaunti ya madeni ya nje EPA wakiwa Mahakamani..

Wednesday, November 5, 2008

Baada ya kutangazwa Ushindi wa Obama..

Raisi mtarajiwa wa Marekani Bw. Barack Obama na Mke wake Michelle Obama wakiondoka ktk mkutano wa kutoa shukurani zao kwa wapiga kura wa Chicago kwa kufanikisha ushindi wa chama chake katika jiji hilo..

Mama huyu wa jiji la New York akilia katika kule kutoamini kama kweli Obama ameibuka kidedea..

Mamia ya wafuasi wa Bw. Obama wakipigwa na Butwaa huku wengine wakiwa na furaha kwa kutoamini ushindi wa mgombea wao..

Nao wakazi wa Kibera nchini Kenya wakifurahia ushindi huo huku wakipeperusha bendera ya Marekani, Kenya ndio asili ya baba yake Obama, Marehemu Barack Hussein Obama..

Mamia ya wafuasi wa Barack Obama wengi wao wakiwa na asili ya weupe wakifurahia ushindi wa mgombea wao.

Raisi mtarajiwa wa Marekani kutoka chama cha Demokratik Bw. Barack Obama akiwa amekumbatiana na mkewe Michelle huku makamu wake Bw. Joe Biden na mkewe wakiwa wamekumbatiana pembeni yao katika kujipongeza kutokana na kuibuka washindi katika kinyang'anyiro cha uraisi nchini humo.

Raisi wa Afghan Bw. Hamid Karzai akiongea na waandishi wa habari ndani ya makazi ya Raisi mjini Kabul, Afghanistan, Jumatano, Nov. 5, 2008. Karzai alisema uteuzi wa Barack Obama kama raisi wa kwanza mweusi wa Marekani ni kiashirio cha wakati mzuri kwa Marekani na Dunia kiujumla..

OBAMA 'Changes has Come to America'

Barack Obama akipungia mkono mamia ya wafuasi wake huku akiwa na Mkewe pamoja na watoto wao katika moja ya kampeni zake za kuwania uraisi wa Marekani, Seneta huyo ameibuka kinara katika kinyang'anyiro hicho kilichokuwa na upinzani mdogo dhidi ya mpinzani wake John McCain kutoka chama cha raisi anayeondoka madarakani Bw. George Walker Bush.

Hatimaye mkenya, Seneta Barack Obama wa chama cha Demokrati cha atinga katika ikulu za marekani, Bw. Obama anaweka historia ya kuwa Mwafrika wa kwanza kuingia katika Ikulu za Marekani maarufu kama 'White House' akiwa raisi wa arobaini na nne (44) kwa Taifa hilo lililo na nguvu zaidi duniani, Obama anaweka historia ya iliyokuwa 'ndoto' ya wanaharakati wengi waki-Afrika akiwemo Martin Luther King Jr na Malcolm 'X' ambao hawakuwahi kutimiza ndoto hiyo waliyoipigania katika kipindi chote cha Uhai wao..

Tuesday, November 4, 2008

Jirambe ndani ya Rock City (Mwanza)

Vijana wa Nyumba ya vipaji Tanzania THT, wakinesa kwa mbwembwe ktk harakati za kuwarambisha urojo wana Rock City, Vijana hawa wameonesha mbwembwe za ajabu toka mwanzo wa Msafara wa Jirambe ulioanzia kule jijini Tanga mpaka hapa ulipofikia..

Wana wa Kiumeni TMK wakiongozwa na Juma Kassimu (Nature a.k.a Kibra) wakishambulia ipasavyo ktk kukonga nyoyo za wananchi waliojitokeza kujiramba ndani ya Viunga vya Yatch Club jijini Mwanza..

Kr Mulla akichizisha wakazi wa Mwanza waliojiachia ndani ya tamasha Fiesta Jirambe Ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza..

Habari Iliyovunjika (Breaking News)

Habari zilizojiri, zinahabarisha kuwa Bibi wa mgombea urais wa Marekani 'Barack Obama' amefariki ikiwa ni siku moja kabla ya uchaguzi wa nchi hiyo, Madelyn Dunham, 86, alikuwa akiugua kansa, Bibi huyo ndio uliokuwa mhimili wa maisha ya utotoni ya Bw. Obama mpaka alipofikia sasa. bonyeza hapa kwa habari zaidi

AY, LADY JD na PAM AWARDS

Washindi katika tuzo maarufu zijulikanazo kama 'Pam Awards' zilizofanyika nchini Uganda jumamosi iliyopita pale Shimoni Grounds.

AY ameibuka mshindi katika kipengele cha Best Male Artist-Tanzania ambapo alikuwa sambamba na wasanii wengine maarufu wa nchini Tanzania kama vile Prof Jay, Mr.Nice na Bushoke huku Lady Jay Dee akiibuka Best Female Artist kutoka Tanzania.

NB: AY (pamoja na MwanaFA) wameteuliwa kuwania KISIMA AWARDS ambazo ni tuzo maarufu za nchini Kenya. Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika tarehe 29 November 2008 jijini Nairobi. AY na MwanaFA wamechaguliwa kuwania tuzo hizo katika kipengele cha Best Video -Tanzania kupitia video yao ya Nangoja Ageuke.

Monday, November 3, 2008

Mbinu mpya ya kuzuia Uhalifu wa Kimtandao

Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Bw. Suleimani Kova amesema jeshi hilo limejizatiti katika kukabiliana na mbinu mpya zinazofanywa na wahalifu wanaotumia mitandao ya kompyuta. Hatua hiyo ya jeshi la polisi imekuja kufuatia kuibuka kwa wimbi la watu wanaotumia mitandao ya kompyuta kuchafua watu ambapo amesema polisi imeamua kufungua barua pepe ambayo itatumika katika kukabiliana na uhalifu wa aina hiyo.

Mambo ya 'EXTREME PARTY'

Chidi Benz na Mr Blue wakikamua katika Extreme Party..

Msanii Cindy kutoka Uganda naye alikuwepo katika kuweka mambo sawa, Cindy ni mmoja kati wasanii wa Kundi la Blu 3 lililotamba sana Afrika ya Mashariki.


Dj Bush Baby akisugua mambo yake kama kawaida, hii ni katika Tigo Extreme Party iliyofanyika ndani ya fukwe CINE CLUB.