Kupitia hapa utaweza kupata Habari mbalimbali zikiwemo za Siasa, Michezo, Biashara, Dini, Mapenzi, Afya, Mazingira na mambo mengi yanayomzunguka mwanadamu.
Sunday, October 26, 2008
Prezzo akimpigia debe 'Obama' kiaina..
Mkali wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Kenya, CBM-Prezzo, yuko katika harakati kubwa za kumpigia kampeni mgombea wa urais nchini Marekani, Barack Obama ambaye asili yake ni Kenya, Prezzo alisema iwapo Obama atashinda kuna manufaa makubwa kwa maendeleo ya Afrika na Dunia nzima kwa ujumla, hivyo anahitaji kuungwa mkono na watu wengi mahali popote Duniani. “Tunaamini kuwa akishinda basi hataweza kusahau nyumbani kwake Kenya na Afrika kwa ujumla. Atakuwa si Rais wa Marekani tu bali Rais wetu sote. Ni mweusi mwenzetu hivyo tunahitaji kumpa sapoti ya kutosha ili ulimwengu umtambue”, alieleza Prezzo alipokuwa ziarani Bongo katika tamasha la College Bash lililofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment