Sunday, October 26, 2008

Odemba kurudisha Heshima?


Mrembo Miriam Odemba kwa mara nyengine tena amekabidhiwa bendera ya nchi akiwa kama Miss Earth Tanzania, baada ya kuharibu ile ya Face of Tanzania, je ataweza rudisha heshima kama ile tena? Miriam ambaye ni mzoefu katika masuala ya uanamitindo ameanza mashindano ya Miss Earth, Phillipines ambapo ameweza kuwa kivutio kikubwa kwa wananchi wa pale. Hivi karibuni, Miriam aliungana na washiriki wenzake katika maonyesho ya mavazi yaliyofanyika katika jengo la duka la Robinson Mall. Miriam hivi sasa anatabiriwa na wataalamu wengi kufanya vizuri katika mashindano hayo kutokana na kile walichosema ni mvuto wa sura, uwezo wa kutembea jukwaani na kujiamini katika mahojiano na vyombo vya habari. "Tanzania imetoa mrembo ambaye ameonyesha umahiri mkubwa" aliandika Marco Ramirez ambaye ni mtaalamu wa masuala ya urembo Philippines. "Huyu (Miriam Odemba) amenishtua sana. Ni mshiriki ambaye ni mmoja wa washiriki washindani wa kunyakua taji. Uchangamfu wake ndio unanifanya nimpe nafasi.” Mashindano ya Miss Earth yatafikia kilele tarehe 9 Novemba huko Manila, Phillipines ambapo warembo 93 watawania taji la Miss Earth na mataji mengine. Miss Earth pia ina mashindano mengine madogo yanayomwezesha mshiriki kujizolea umaarufu na zawadi ndogondogo kama taji la vazi la ufukweni, kipaji na nguo ya jioni

No comments: