Friday, October 31, 2008

Hotuba kwa taifa leo, JK kutoka vipi?


Kama alivyozoeleka?!

Hotuba kwa taifa leo, JK kutoka vipi?


Ama hii iliyo nadra kuonekana?!?

Mrithi wa Chacha Wangwe Aapishwa Bungeni


Bw. Mwera Nyanguru aliyeshinda kiti cha Ubunge wa wilaya ya Tarime kupitia tiketi ya chama cha Chadema, akiapa bungeni kuendelea na nafasi iliyoachwa na marehemu Chacha Zacharia Wangwe..

Thursday, October 30, 2008

Ni wakati wa ku-Freeze


Ambwene Yessayah. Maarufu kama 'A.Y' huku wengine wakimuita “Mzee wa Commercial”. Mafanikio yake katika muziki ni mfano wa kuigwa na wengi hasa kwa wasanii chipukizi, A.Y ni miongoni mwa wawakilishi wazuri wa Tanzania nje ya nchi kupitia sanaa ya muziki. Kwa mara nyingine tena mwaka huu anawania tuzo maarufu za Kisima za nchini Kenya.
Kwa sasa jamaa anatamba na kibao kinachoenda kwa jina la 'Freeze' akiwa ameshirikiana na wakali 'P Square' wazee wa 'Do me' kutoka nchini Nigeria. Wimbo umetayarishwa na kurekodiwa na Producer 'Hermy B' kutoka Tanzania, na kuna tetesi kuwa video yake inatarajiwa kufanyika nchini Nigeria na baadhi ya nchi nyingine za Afrika ikiwemo Tanzania. Tayari wimbo huu unakamata chart katika vituo mbalimbali vya radio hapa nchini na huko Nigeria..

Wednesday, October 29, 2008

Tafrani la wana Jumuiya ya Afrika Mashariki..

Baadhi ya wakazi wa Jijini, wakishindwa kuvuka kuja mjini leo asbh kutokana na Wazee wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuziba barabara ya Ali Hassan Mwinyi katika eneo la Salender Bridge leo Asbh..

Wastaafu wa iliyokuwa East Africa Community (Jumuiya ya Afrika Mashariki) leo alfajiri majira ya saa 1:00, walijitokeza na kufunga barabara ya Ali hassan Mwinyi eneo la daraja la Salender katika kuishinika serikali iweze kuwalipa mafao yao, Wazee hao baadhi walikuwa wanapiga mayowe, wengine walionekana wakisali na hata wengine walisaula viwalo vyao katika kuonyesha machungu waliyonayo kutokana na kutolipwa viinua mgongo vyao kwa kipindi kirefu. Tukio hilo liliweza kushuhudiwa na Mkuu wa mkoa wa dar es salaam Bw. Abass Kandoro, na Kamanda wa kikosi cha kanda maalum Bw. Suleiman Kova..

Nyamaza...

Kama muwaonavyo wanamsafara wa Fiesta jirambe, wakiwa ktk moja ya pozi zao katika Picha.. Msafara huo kwa sasa unaelekea Mwanza 'Rock City' ambako kutawaka moto si wakitoto, kwani kutakuwa na wasanii wengi kuliko mikoa mingine iliyowahi iliyopitiwa na Msafara huo unaozunguka karibu nchi nzima ktk kuendeleza ule utamaduni wa wasanii...

Pantoni lakwama Dar..

Kimbembe kilichotokana na kukwama kwa kivuko cha Mv Kigamboni kimezuka leo asbh na kusababisha kero kubwa ya usafiri miongoni mwa wakazi wa Kigamboni, hali hiyo ilitokana na kutitia mchangani kwa kivuko hicho kikubwa kinachotegemewa kuvusha watu wa eneo hilo, Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Pantoni hilo lilikwama toka alfajiri kutokana na kinachodaiwa kuwa nahodha wa wake kuchelewa kukiondoa kabla maji kupwa. mashuhua waliendelea kunyetisha kuwa kutokana na kivuko hicho kikubwa kukumbwa na tatizo hilo, wasafiri wakawa wakitegemea kivuko kidogo cha Mv Alina, hali iliyoendelea kuzua tafrani kwani abiria walikuwa wengi kuliko kivuko hicho...

Fiesta Jirambe ndani ya Dom

Halikuwa jambo la Ajabu kushudia kila mtu akijiramba kwa staili yake, hapa jamaa akichumpa kutoka jukwaani..

Wakazi wa Dom walifurika kama uonavyo katika kujiramba kwa nafasi.. Hii ni sehemu tu ya Umati wa raia waliofurika katika Viwanja vya Jamhuri kushuhudia ma mambo ya Fiesta 'Jirambe'
Tamasha la fiesta jirambe 2008 lilivyokuwa pande ya wakazi wa Dodoma, wakazi wa Dodoma wanajua kujiramba ile kisawa sawa, jana jirambe ilikuwa inafanyika ndani ya uwanja wa mpira wa Jamhuri, wasanii chipukizi walianza kupanda jukwaani kuanzia majira ya saa sita na kitu hivi na baadaye wakongwe waakaanza kuwarambisha madude havi wakazi wa Dom, palikuwa hapatoshi uwanjani hapo. Pichani kama uonavyo umati wa wakazi wa Dodoma ulivyoamua kujiramba kwa staili ya aina yake..

Tigo na Xtreme Party


Afisa Uhusiano wa Tigo akitangaza mpambano wa DJ's na wasanii wa Afrika Mashariki utakaojulikana kwa jina la Xtreme Party mpambano huo unatarajiwa kufanyika katika fukwe za Cine Club maalum kwa wateja wa kudumu wa Tigo kuanza kufurahia mwisho mzuri wa mwaka 2008.

Kushoto kwake ni msanii wa Bongo flava Herry Sameer (Mr Blue) na Ruta Bushoke watakaoshiriki kuiwakilisha Tanzania. wasanii wengine watakaoshiriki mpambano huo ni kundi zima la P Unit kutoka Kenya na aliyekuwa muimbaji wa kundi la Blue 3 mwanadada Cindy nani atakaeibuka XTREME. Kwa mpambano wa DJ' atakuwepo Bush Baby na Wesley kutoka Kenya.

Wahariri waandamana Dar

Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wameandamana jijini Dar es salaam, maandamano hayo yalianzia mtaa wa Lugoda na kuelekea wizara ya habari utamaduni na michezo, ambako walikabidhi barua kwa Waziri wa wizara hiyo Mh George Mkuchika, aidha madhumuni ya maandamano hayo yalikuwa ni kupinga kufungiwa kwa gazeti la mwanahalisi na serikali kwa muda wa miezi 3 na pia kuishinikiza serikali ifanye marekebisho ya sheria ya uhuru wa vyombo vya habari ya mwaka 1976.

Monday, October 27, 2008

Mnyama Simba apigwa Moja

Mechi kali kati ya watani wajadi, Simba na Yanga imekwisha na matokeo ni kwamba Simba imelimwa bao 1-0 lililofungwa na Ben Mwalala katika Dk. 16. Pambano hilo lililofanyika kwa mara ya kwanza kwenye uwanja mpya wa kisasa jijini Dar es salaa na lilitawaliwa na ubabe miongoni mwa wachezaji ambapo refa alilazimika kutoa jumla ya kadi nyekundu 3, mbili kwa Simba, moja kwa Yanga..
Kikosi kilichouwa Mnyama kikielekea mapumzikoni..

na mashabiki nao hawakuwa nyuma ktk kushangilia mauaji ya mnyama Simba...

Sunday, October 26, 2008

KLM wazindua Boeing 777


Shirika la Ndege la KLM la uholanzi, leo linatambulisha yake ndege aina ya Boeing 777 inayotarajiwa kutua usiku huu tayari kwa kuanza safari zake kupitia Dar, utambulisho huu umepambwa na kikundi cha ngoma cha Steel of Heaven (Mapipa ya Mbinguni) cha Kurasini kilichoonyesha umahiri wa kupiga nyimbo mbalimbali maarufu hapa nchini wakitumia mapipa.. Pichani ni mfano wa ndege hiyo ambayo imeshatambulishwa nchi nyingi za bara Ulaya, Sherehe hizo zilifanyika katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA)

Rudy Ray Moore Afariki Dunia


Mmoja wa wachekeshaji wa Marekani mwenye asili ya kiafrika, Rudy ray Moore amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 81 baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kisukari. Ruudy Moore ambaye pia anafahamika kama baba wa muziki wa rap nchini humo, aliwahi kutamba katika vichekesho na muziki wa rap mwanzoni mwa miaka ya 1970. baadi ya vipindi vya vichekesho vilivyowaahi kutamba ni pamoja na Delomite, The human Tornado, Money Hustler, The devil's son in Law na Petey Wheatstraw, Moore alizaliwa Machi 17 mwaka 1927, kabla ya kugeukia mziki awali alikuwa Mwanajeshi..

Mungu ailaze Roho Rudy mahali pema peponi... Amen

Prezzo akimpigia debe 'Obama' kiaina..

Mkali wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Kenya, CBM-Prezzo, yuko katika harakati kubwa za kumpigia kampeni mgombea wa urais nchini Marekani, Barack Obama ambaye asili yake ni Kenya, Prezzo alisema iwapo Obama atashinda kuna manufaa makubwa kwa maendeleo ya Afrika na Dunia nzima kwa ujumla, hivyo anahitaji kuungwa mkono na watu wengi mahali popote Duniani. “Tunaamini kuwa akishinda basi hataweza kusahau nyumbani kwake Kenya na Afrika kwa ujumla. Atakuwa si Rais wa Marekani tu bali Rais wetu sote. Ni mweusi mwenzetu hivyo tunahitaji kumpa sapoti ya kutosha ili ulimwengu umtambue”, alieleza Prezzo alipokuwa ziarani Bongo katika tamasha la College Bash lililofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

'College Bash' ilivyopagawisha

Usiku wa kuamkia leo latika Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam, kulikuwa na Tamasha la Muziki lililojumuisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali al maarufu kama 'College Bash' ambapo wasanii mbalimbali kutoka nchi jirani za Kenya, Uganda na hapa nchini walikonga nyoyo za mashabiki wao ipasavyo.

Ambwene Yesaya maarufu kama AY aliweza kuwakimbiza mchakamchaka wasanii waalikwa..

Mrembo akipiga mwereka mbele ya Msanii Nameless kutoka Kenya ktk harakati za kumsapoti..

Lord Eyez wa Nako 2 Nako akifanya makamuzi jukwaani, Msaani huyu na kundi lao walibamba vilivyo madenti waliofurika ukumbini humo..

Duh!

Mambo ya Fiesta 'Jirambe'

Qchila nae akikamua vilivyo mbele ya wakazi wa Moro,Chila bila hiyana aliutambulisha wimbo wake mpya kabisa uitwao Paparazi ambao ulionekana kuwakuna mno washabiki waliotinga ukumbini humo


Pichani ni wasanii wa Nyumba ya Vipaji Tanzania maarufu kama THT au kwa kirefu Tanzania House of Talent wakiwa jukwaani kwenye tamasha la Fiesta Jirambe 2008.

Msafara wa Fiesta Jirambe Moro

Wasanii mbalimbali walioko kwenye msafara wa tamasha la Fiesta 'JIRAMBE' kwa kushirikiana na waandaji wake Prime Time Promotions na Clouds Fm walikwenda kutoa msaada wa vyakula kwenye kambi ya Walemavu pamoja na wazee wasiojiweza kiitwacho funga funga kilichopo kota za reli Morogoro . Pichani ni mkuu wa msafara huo Bw. Cosmo ambaye ni mtangazai wa Clouds fm kupitia kipindi cha reggae kinachorushwa kila siku ya Ijumaa usiku akijitambulisha mbele ya wazee hao (hawako pichani) pamoja na wageni wasanii alioongozana nao.

JK ahani msiba wa Watoto Tabora

Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana amekutana na kuwapa pole binafsi wananchi wa mjini Tabora, ambao mwanzoni mwa mwezi huu walifiwa na watoto wao 19 katika tukio la kusikitisha kwenye Sikukuu ya Idd El Fitr, Oktoba Mosi, mwaka huu.

Rais, ambaye ameanza ziara ya kikazi ya siku nane ya mkoa huo, amekutana na wazazi na walezi 16 wa watoto hao waliopoteza maisha kwenye ajali ya kubanana kwenye ukumbi wa disco wakati ulipotokea moto kwenye ukumbi huo kwenye jengo la NSSF mjini Tabora.

Watoto wengine 16 walilazwa hospitali kutokana na kuumia katika tukio hilo. Mpaka sasa wote wametibiwa na kuruhusiwa kurejea nyumbani, isipokuwa mmoja ambaye amehamishiwa Hospitali Kuu ya Taifa ya Muhimbili, Dar Es Salaam, kwa matibabu zaidi.

Baada ya kuwa amempa mkono kila mfiwa katika tukio hilo nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, mjini Tabora Rais amewaambia wafiwa hao:

“Siku ile ya Idd El Fitr, nilipata habari za kusikitisha za msiba wa watoto wetu. Nikamtuma Waziri Kapuya (Profesa Juma Athuman Kapuya – Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana) kuja kuungana nanyi kwa niaba ya Serikali kwenye msiba huu. Lakini maadamu nimepata nafasi ya kuja hapa mwenyewe, nimeona ni jambo zuri nikutane, ili niweze kuwapeni pole mimi binafsi.

Ameongeza Rais: “Nataka mjue kuwa msiba wenu, ni msiba wetu sote. Majonzi yenu, ni majonzi yetu, Masikitiko yenu, ni masikitiko yetu. Kila mzazi hupenda mtoto wake aweze kukua na kumzika yeye. Lakini pia Mwenyezi Mungu ana mipango na maamuzi yake. Nawapeni pole na kuwafariji wa namna ya pekee.”

Wazazi hao nao wamemshukuru Rais Kikwete binafsi, na uongozi wa wilaya ya Tabora na mkoa wa Tabora kwa namna ya pekee ambayo walishiriki katika kuwafariji wakati wa msiba huo mkubwa.

Mara baada ya kutokea ajali na msiba huo, Rais alitoa ubani wa sh 500,000 kwa kila mototo aliyepoteza maisha na sh 100,000 kwa kila mtoto aliyeumia.

Miongoni mwa watu wengine ambao walitoa ubani ni mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, na Mbunge wa Igunga, mkoani Tabora, Rostam Aziz.

Ngeleja akabidhi mradi wa Umeme Salasala


Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngeleja amekabidhi Mradi wa umeme uliopo kijiji cha Salasala uliojengwa chini ya mradi wa uendelezaji wa gesi ya asili ya Songosongo sherehe hiyo iliambatana na kukabidhi miradi mingine waliyoijenga ambayo ni maji, barabara na simu, katika maeneo ya Salasala na Kinyerezi. Hafla hiyo ilifanyika maeneo ya Salasala nje kidogo ya jiji la Dar, Aidha Wilaya hiyo imejengewa barabara tano za lami zenye urefu wa kilomita sita na nusu.

Odemba kurudisha Heshima?


Mrembo Miriam Odemba kwa mara nyengine tena amekabidhiwa bendera ya nchi akiwa kama Miss Earth Tanzania, baada ya kuharibu ile ya Face of Tanzania, je ataweza rudisha heshima kama ile tena? Miriam ambaye ni mzoefu katika masuala ya uanamitindo ameanza mashindano ya Miss Earth, Phillipines ambapo ameweza kuwa kivutio kikubwa kwa wananchi wa pale. Hivi karibuni, Miriam aliungana na washiriki wenzake katika maonyesho ya mavazi yaliyofanyika katika jengo la duka la Robinson Mall. Miriam hivi sasa anatabiriwa na wataalamu wengi kufanya vizuri katika mashindano hayo kutokana na kile walichosema ni mvuto wa sura, uwezo wa kutembea jukwaani na kujiamini katika mahojiano na vyombo vya habari. "Tanzania imetoa mrembo ambaye ameonyesha umahiri mkubwa" aliandika Marco Ramirez ambaye ni mtaalamu wa masuala ya urembo Philippines. "Huyu (Miriam Odemba) amenishtua sana. Ni mshiriki ambaye ni mmoja wa washiriki washindani wa kunyakua taji. Uchangamfu wake ndio unanifanya nimpe nafasi.” Mashindano ya Miss Earth yatafikia kilele tarehe 9 Novemba huko Manila, Phillipines ambapo warembo 93 watawania taji la Miss Earth na mataji mengine. Miss Earth pia ina mashindano mengine madogo yanayomwezesha mshiriki kujizolea umaarufu na zawadi ndogondogo kama taji la vazi la ufukweni, kipaji na nguo ya jioni

Wateule wajipanga Upya


Yawezekana kuwa si jambo lililotarajiwa kutokea ktk siku za karibuni,lakini ukweli ni kwamba kundi la 'Wateule' linarejea upyaaaa....na tayari memba waliokuwa wakiunda kundi hilo tayari wamemesharekodi nyimbo nne. Unaweza usiamini kinachotokea lakini Jahffarai ambaye alikuwa akiongea kwa niaba ya wenzake anasema.... "Pini ambazo tumesharekodi hadi hivi sasa ni 'Tumetoka Mbali`, `Msela`, `Bado Yuko Vilevile` na `Mtaani Kuna Njaa`.....na albam inakuja,`` . Rapa huyo alisema ufufuko huo wa Wateule unahusisha muungano mpya wa memba wa kundi hilo - Jaymoe, Mchizi Mox, Kevin Kimali, yeye mwenyewe Jaffarai na Solo Thang ambaye kwa sasa anaishi Uingereza. .....``Katika pini hizi za kwanza tumerekodi sisi wanne bila ya kumshirikisha Solo Thang, lakini mipango inafanywa ili kumtumia beats ili atie mistari yake katika nyimbo zinazofuata. ``Marejeo haya ni `sirias` na tunatarajia kuwashirikisha wakali wa Afrika Mashariki kwa kuwa lengo letu sasa ni kusonga mbele.`` ``Ninapokwambia kuwa marejeo haya ni `sirias` ni kwamba ninamaanisha hivyo, wakati wowote tutaanza kurekodi video yetu ya kwanza ya wimbo wa `Mtaani Kuna Njaa` na muda mfupi baadaye tutaachia pini la kwanza la utambulisho katika vituo vya radio,`` alisema Jaffarai. ``Tumeungana kufanya kazi pamoja kwa mara nyingine kwakuwa tunafahamu nguvu kubwa iliyokuwepo ya kundi letu kabla ya kumeguka. Nadhani unaweza kuwa na japo picha ya nini kitatokea vinapokaa vichwa hivi pamoja,`` alisema. Kuungana upya kwa memba wa Wateule kunaashiria jambo. MWAKA WA MALAIKA? Pengine `mwaka wa shetani` ulioimbwa na rapa wa TMK Wanaume Family Mheshimiwa Temba baada ya kushuhudia makundi kibao yakivunjika umefikia tamati. Pengine TMK Wanaume Family na Wanaume Halisi nao wataungana upya mwaka huu, au MwanaFA na AY watarejea kwa kamanda wao wa zamani King Crazy GK wa EastCoast Team. Au Ferooz na Daz Baba wataungana tena kuliteremsha upya majini jahazi lao la Daz Nundaz. Nani ajuaye ya kesho? Lakini kuungana upya kwa Wateule, bila ya shaka, ni jambo ambalo lilikuwa likisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa hip hop kwasababu wanajua. Wanajua nini wanachotarajia kutoka kwa wakali hao wa mistari waliotambulishwa katika gemu mwaka 2000 kupitia wimbo wao wa ?Hip Hop na Ragga?. WATU KIBAO Wimbo wa `Hip Hop na Ragga` ulikuwa ni kazi ya kwanza na ya mwisho kubwa kwa kundi hilo ambalo liliundwa baada ya wakali hao kukutana kwa mtayarishaji wa muziki P-Funk kwa lengo la kurekodi nyimbo - kila mtu wa kwake - kufuatia ofa waliyopata baada ya kushinda mashindano ya vipaji vya muziki ya Pilsner Ice Pop Stars 2000. Kundi la Sower Cellibas lililoundwa na Jaymoe, Mchizi Mox na Kevin Kimali lilikuwa limeshinda katika kategori ya hip hop, na Solo Thang aliibuka wa pili baada ya kuyapiku makundi na wasanii mbalimbali kama HBC, BDP na Inspektah Haroun. Mark II B alikuwa wa kwanza katika kategori ya Ragga akifuatiwa na Lady Lou, katika mashindano hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mambo Club. ``Ushindi wa kila msanii ama kundi ulitupatia nafasi ya kurekodi wimbo katika studio ya Bongo Records,`` anakumbuka Jaffarai. ``Lakini tukiwa pale studio kwa ajili ya kurekodi wimbo kwa kila mshindi, prodyuza P-Funk alionekana kama kuingia hofu kama tutaweza kufanya vizuri kama kila mmoja atarekodi kivyake, akatushauri turekodi pamoja. ``Kwa sababu ulikuwa ni muunganiko wa wasanii wa hip hop na wa ragga, tukaamua kuuita wimbo huo ?Hip Hop na Ragga`. ``Baada ya kurekodi na prodyuza kukubali kuwa `pini` limetulia, alitushauri tutafute jina na tuendelee kufanya kazi pamoja. ``Wakati tukijiuliza tutumie jina gani, ndipo Kevin Kimali alipotoka na jina hili la Wateule akimaanisha washindi baada ya shindano la pop stars. ``Kundi likaundwa na wasanii saba Mchizi Mox, Kimali, Solo Thang, Jaymoe, Lady Lou, Mark II B na mimi (Jaffarai).`` Muda mfupi baadaye, Solo Thang akajitoa ili afanye kazi kivyake, akifuatiwa na Jaymoe, Lady Lou na Mark II B na kuwaacha wasanii watatu - Mox, Jaffarai na Kimali - ambao wakarekodi katika studio ya MJ Records nyimbo za `Nipende Nichukie`, na ?Watu Kibao? iliyowatoa kiukweli. Katika marejeo, Wateule hawajasahau njia walizopitia awali. Ndiyo maana wamerekodi kwa MJ na pia kwa P-Funk. ``Na tuna nyimbo tutazirekodi nchini Kenya na Uganda,`` alisema Jaffarai. Hata hivyo Jahffarai anasema kurejea kwao hakutawashirikisha wenzao wawili Lady Lou na Mark II B...ambao wao wameamua kukaa mbali na muziki kwa miaka mingi sasa.

Tanzania Information and History


Tanzania, the largest country in East Africa, includes the spice islands of Zanzibar, Pemba, and Mafia and contains Africa's highest point—Kilimanjaro, at 5,895 meters (19,340 feet). Kilimanjaro, a dormant volcano, is snowcapped even though it is near the Equator. The African population consists of more than 120 ethnic groups.

Tanganyika, a British-controlled UN trust territory, gained independence in 1961; and Zanzibar, a British protectorate with an Arab population, became independent in 1963. Tanganyika and Zanzibar united to form Tanzania in 1964. Until resigning as president in 1985, independence leader Julius K. Nyerere guided two decades of socialism—adapted to the ujamaa policy of village farming. A multiparty system was established in 1992 after a constitutional amendment.

Some 80 percent of Tanzanians farm or fish at subsistence levels; in many areas tse-tse fly infestation hampers successful animal husbandry. Deteriorating roads and railways and high energy costs are major problems. The Ngorongoro Crater and Serengeti National Park are rich in wildlife, although poaching endangers some species. Tourism remains important. Dar es Salaam is the administrative capital, but Dodoma is the designated future capital and current home to Tanzania's legislature.

ECONOMY Industry: agricultural processing (sugar, beer, cigarettes, sisal twine), diamond and gold mining, oil refining. Agriculture: coffee, sisal, tea, cotton; cattle. Exports: gold, coffee, cashew nuts, manufactures, cotton.