Miili nyumba walikuwa na kazi ya ziada kwani mwanadafada Eve alikuwa hakamatiki kwa kujichanganya na mashabiki kila mzuka unapompanda, Hii nadhani ni baada ya kuona kila upande umejaa ngozi yenye rangi yake ya asili..
Mtu mkubwa kutoka Terror Squad, FAT JOE! akishambulia jukwaa ndani ya viwanja vya Gymkhana jijini Dar katika Tamasha la Likizo Tym lifanyikalo karibu kila mwishoni mwa Mwaka.
Kumbe ile tabia ya mikono ya kushoto ya wasanii walio wengi kushika katika maeneo haya kuhu wakiwa wameinama kidogo hata akina dada wanayo jamani!? Ila hii nimeiona sana kwa wale wasanii wenye miondoko ya kughani/kufokafoka 'Rap/Hip Hop' na ni aghalabu sana kuwakuta wasanii wakuimba wakikamata maeneo hayo..
Naahidi kuweka picha zaidi za washika huko kwani inaonekana ni kama kaji-jadi flani hivi kwa upande wao!
No comments:
Post a Comment