Friday, December 12, 2008

TID kubadili Jina..

Msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya hapa Tanzania, Khaleed Mohamed 'Top In Dar' a.k.a TID amechukua uamuzi huu baada ya kutoka gerezani katikati ya wiki hii kutokana na msamaha wa Rais JK, Kwa sasa msanii huyo ataanza kutambulika kwa jina la Prison Voices.
Pichani juu ni TID akiwa katika moja ya matamasha yake aliyowahi kufanya akiwa nje ya nchi..
I wish U all the Best Home boy..

Wednesday, December 10, 2008

Makamuzi ya EVE na FAT JOE ndani ya Bongo 'Likizo Tym'

Miili nyumba walikuwa na kazi ya ziada kwani mwanadafada Eve alikuwa hakamatiki kwa kujichanganya na mashabiki kila mzuka unapompanda, Hii nadhani ni baada ya kuona kila upande umejaa ngozi yenye rangi yake ya asili..


Mtu mkubwa kutoka Terror Squad, FAT JOE! akishambulia jukwaa ndani ya viwanja vya Gymkhana jijini Dar katika Tamasha la Likizo Tym lifanyikalo karibu kila mwishoni mwa Mwaka.


Kumbe ile tabia ya mikono ya kushoto ya wasanii walio wengi kushika katika maeneo haya kuhu wakiwa wameinama kidogo hata akina dada wanayo jamani!? Ila hii nimeiona sana kwa wale wasanii wenye miondoko ya kughani/kufokafoka 'Rap/Hip Hop' na ni aghalabu sana kuwakuta wasanii wakuimba wakikamata maeneo hayo..
Naahidi kuweka picha zaidi za washika huko kwani inaonekana ni kama kaji-jadi flani hivi kwa upande wao!

Hamasisho la siku ya UKIMWI duniani


Katika katizakatiza zangu mitandaoni nimekumbana na picha hili linalosisitiza matumizi ya kondom katika kuhamasisha matumizi ya kifaa hicho, Picha hiyo ni maalum kwa ajili ya siku ya Ukimwi Duniani yaani kila tarehe 9 ya mwezi wa 12 wa kila mwaka.
Swali ni Je? Hicho kidole kilicho na pete si ni mahsusi kwa ajili ya wana ndoa si ndio? Sasa inamaana hao wanandoa hawatumii kivazi 'Kondom' na ndio wako salama zaidi?

Tuesday, December 9, 2008

Eve/Fat Joe ndani ya Likizo Tym

Hapa Fat Joe akiteta jambo na Eve mara tu walipokutana katika viunga vya hoteli ya Kilimanjaro Kempisk

Mwanamuziki nguli kutoka katika kundi la Terror Squad, Fat Joe, akihojiwa na baadhi ya waandishi wa habari kutoka Cloudz FM alipokuwa akiwasili ndani ya viwanja vya Kilimanjaro Hotel Kempisk, Fat na EVE wako nchini kwa ajili ya tamasha la Likizo Tym.

EVE akiongea na wanahabari pamoja na raia kadhaa walioalikwa katika pati ya Meet & Greet ndani ya Hotel ya Kilimanjaro Kempisk.